Bongo 5 Tanzania

DC wa Kibaha, Bi Assumpter Mshana atinga ofisi za Osha na ujumbe huu

Mkuu wa Wilaya Kibaha Mh Assumpter N. Mshama ameipongeza OSHA kwa kusimamia utekelezaji wa sheria ya Usalama na Afya Mahali pa kazi nchini kwa kufika sehemu kubwa wilaya humo.

Akizungumza mara baada ya kutembelea Ofisi za OSHA jijini Dar es salaam, Assumpter amesema ameamua kutembelea katika ofisi hizo ili kutoa pongezi kwa ushirikiano mkubwa walioupatia Wilaya hiyo kutokana zoezi la ukaguzi wa maeneo ya kazi hususani Viwanda vilivyopo Wilayani Kibaha kuona utekelezaji wa sheria ya usalama na Afya mahali pa kazi

Aidha Mkuu huyo wa Wilaya, amewataka wamiliki wa Viwanda Wilayani Kibaha kuhakikisha wanazingatia sheria ya usalama na Afya Mahali pa Kazi, ili kulinda nguvu kazi, na kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli, katika ujenzi wa Viwanda.

Mshama ameongeza kuwa Katika kuunga juhudi hizo ambapo pia nchi za SADC zimemuunga mkono Mh Rais John Pombe Magufuli, katika zima za ujenzi wa Viwanda nchini.

Naye Kaimu Mtendaji Mkuu wa OSHA Bi Khadija Mwenda, amesema wataendelea kusimamia sheria ya usalama na Afya kama sheria inavyoelekeza ili kuweza kulinda wafanyakazi katika maeneo ya kazi. Khadija amemshukuru mkuu huyo wa wilaya kuja kutembelea Ofisi za OSHA na kuwapa mrejesho juu ya zoezi maalamu la Ukagauzi lilofanywa na OSHA kwa lengo la kukagua maeneo ya kazi wilaya Kibaha kuona utekelezaji wa sheria ya usalama na Afya, kutokana na Wilaya hiyo kuwa na Viwanda Vingi hapa nchini.

[ad_2]

Source link

Related posts

Rais Kim Jong Un aanza utekelezaji wa adhabu mpya ya kifo aliyojifunza kwenye filamu ya James Bond, Atakayekutwa na hatia kugeuzwa kitoweo

uhondo news

Yaelezwa takribani wafungwa 57 wameuawa kikatili katika gereza moja nchini Brazil

uhondo news

MALAIKA ANATAKA WATU WAPENDWE WAKIWA HAI

uhondo news