WEMA AMKOSESHA RAHA AUNT EZEKIEL

Leo staa wa Bongo Movies, Wema Isaac Sepetu ‘Tanzania Sweetheart’ anatimiza siku ya tano akiwa mahabusu katika Gereza la Segerea jijini Dar, lakini nyuma ya pazia, jambo hilo limemkosesha raha rafiki yake kipenzi, Aunt Ezekiel.

 

Mapema Jumatatu wiki hii, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar iliamuru Wema kupelekwa gerezani Segerea kwa siku saba huku sababu ikitajwa kuwa alikiuka masharti ya dhamana katika kesi ya msingi inayomkabili ya kusambaza picha za ngono mitandaoni.

 

Katikati ya majanga hayo ya Wema, Aunt ambaye mbali na kuwa rafiki yake wa karibu ni mwigizaji mwenzake ameonekana kuguswa mno na amri hiyo iliyotolewa na mahakama.

 

Aunt alionesha kumkumbuka rafiki yake huyo na kuamua kutumia ukurasa wake wa Mtandao wa Instagram kuposti picha nyingi akiwa na Wema na kuandika maneno ya matumaini kwamba ipo siku yote haya yatapita na Wema atabaki kuwa rafiki mzuri kwake.

“Ni vizuri pale watu wasiojuana kuwa marafiki, lakini ni huzuni pale marafiki wawili wanapokuwa hawajuani tena. Wema utabaki kuwa rafiki mzuri kwangu daima, Inshallah hili pia litapita,” aliandika Aunt kwenye ukurasa wake wa Instagram.

 

Wema alikumbwa na msala huo mwishoni mwa mwaka jana ambapo picha zake zilimuonesha akiwa kwenye mahaba mazito na jamaa aliyetajwa kwa jina la Patrick Chrostopher ‘PCK’

Toa comment